Juma Nature Aungana na Afande Sele Kutoa Madongo Kuhusu Wasafi Festival

Mkongwe wa Bongo Fleva Sir Juma Nature amefunguka na kutoa neno kwa mkongwe mwenzake katika tasnia ya Bongo Fleva Simba wa Morogoro Afande Sele.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Nature ameandika ujumbe huo kitu ambacho kinahusishwa na tamasha la Wasafi Festival ambalo linatarajia kufanyika wikiendi hii likitoka mjini Iringa.

download latest music    

Juma Nature kwa asilimia kubwa atakuwepo kwenye tamsha hilo kutokana na kauli aliyoitoa mmoja wa mameneja wa Diamond Mkubwa Fela baada ya kusema ” Mwanangu Juma Nature Kiroboto atakuwepo kwenye Wasafi Festival ya Iringa na Morogoro”

Nature kuitia ukurasa wake wa Instagram ameandika “Mjomba andaa magimbi matamu mwenye chuki anaendelea nachukizake.”

Huu ni muendelezo wa bifu za chini chini zinazoendelea katia ya wasanii  wanaotaka kufanya show na WCB na wale ambao waliotakiwa kufanya show ya fiesta wikiend iliyopita lakini ilishindikana akwa sababu show hiyo ilihairishwa.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.