Loading...

Jux: “Bado nampenda Vanessa”

September 09, 2017 at 14:02
Jux: "Bado nampenda Vanessa"

Mwanamuziki Juma Jux amekiri kuwa bado anampenda mpenzi wake wake wa zamani Vanessa maarufu kama V-money , Jux na Vanessa waliachana miezi mitano iliyopita baada ya kudumu kwenye mahusiano ya kimapenzi kwa muda wa miaka minne.  Jux aliweka wazi  kuwa wimbo wake mpya “Utaniua” aliouachia  hivi karibuni  alimuimbia Vanessa, Lakini katika mahojiano tofauti aliyofanya Vanessa alisema wimbo wake mpya wa “Kisela” ulihusu maisha yake binafsi na hisia alizopitia katika mahusiano yake na Jux.

Katika mahojiano aliyoyafanya Jux hivi karibuni alikiri kuwa bado anampenda vanessa na ataendelea kumpenda na itakuwa ngumu kwake kumsahau na itamchukua muda mrefu sana. Moja kati ya vitu mashabiki wengi wa wasaanii hawa wamekuwa wakijiuliza na wakitaka kujua ni sababu gani iliyopelekea wawili hao kufikia uamuzi huo wa kuachana, Jux aliweka wazi kuwa muda na umbali uliokuwepo baina yao  ulikuwa kikwazo kikubwa katika mahusiano yao na alisisitiza kuwa kati ya yeye na Vanessa hakuna hata mmoja wao aliyechepuka (kuwa na wapenzi wengine).

download latest music    

Jux amesisitiza kuwa yeye na Vanessa hawana uadui wowote na wataendelea kuwa marafiki wa karibu japokuwa saa nyingine bado ni ngumu kwake kumuona Vanessa kwenye mitandao ya kijamii mpaka kufikia hatua ya kuamua “kum-block “. Lakini amekiri kuwa “Vanessa amenifundisha vitu vingi sana na amenipa changamoto sana kwani yeye ni msanii mzuri kwaiyo nilikuwa siwezi nikaona yeye anatoa nyimbo na video nzuri alafu mimi nikabweteka bali alinipa changamoto ya kuwa mtafutaji”

Jux amemalizia kwa kusema hayupo kwenye mahusiano yoyote kwa sasa ameamua atumie muda wake kufanya muziki na pia amekiri akisikia Vanessa ana mpenzi mwingine itamuumiza sana.

Loading…

Share

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment