Jux Kuyaanika Maisha ya Vee Kwenye Zaidi.

MWANAMUZIKI wa Bongo Fleva, Juma Mussa ‘Jux’ hivi karibuni ameachia video yake mpya ya Ngoma ya Zaidi ambayo hadi gazeti hili linakwenda mtamboni kwa upande wa Tanzania ilikuwa ni namba tano kwenye ngoma zinazotrendi.

Simulizi ya video hiyo ni namna ambavyo Jux alikuwa amezama kwenye penzi zito la mwanadada ambaye alikuwa anasomea sheria na anakwenda mtaani kumtafuta alikomuona kwa mara ya kwanza.

download latest music    

Ukiicheki video hii, Jux ni kama ameweka maisha ya mpenzi wake, Vanessa Mdee ‘Vee Money’ ambaye naye ni mwanasheria wa ngazi ya digrii aliyesomea nchini Kenya kwenye Chuo cha Catholic University of Eastern Africa.

Akizungumzua juu ya hilo, Jux alisema: “Wakati ninaandaa namna video itakavyokuwa sikuwaza kuhusu hilo, lakini baadaye ndiye (Vee Money) alifahamu kwamba kwa namna moja au nyingine video hiyo inaendana na ukweli.”

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.