Kajala, Wolper na Harmonize Waingia Katika Bifu Zito

Mastaa wawili wa Bongo movies Kajala Masanja na Jacqueline Wolper wameingia katika bifu zito baada ya maongezi kwa njia ya video ‘video call’ baina ya Kajala na mpenzi wa zamani wa Wolper mwanamuziki Harmonize kuvuja mtandaoni na kuibua makubwa.

Kajala alikuwa akizungumza kwa njia hiyo ya kisasa na Harmonize ambae alionekana akila tunda aina ya apple kitandani kwake huku na Kajala akiwa kitandani kwake, baadaye Harmonize aliirusha picha hiyo mtandaoni na kusababisha minong’ono ya chini chini kusambaa. Picha ile ilimkera Wolper ambaye ametoka kuachana na Harmonize miezi si mingi na Kajala pia ni rafiki yake hivyo ilipelekea Wolper kuandika maneno yafuatayo kwenye picha ile: “Yaani nimekaa hapa mwenyewe nimewaza mapenzi ya siku hizi yana drama mno, mara leo huyu mara kesho yule”. Akijua wazi Kajala ameumizwa na kitendo hicho. 

download latest music    

Wema Sepetu naye aliingilia kati ishu hiyo na kuandika maneno chini ya picha hiyo “Be carefully my baby huyo nyakunyaku asije akapita maana keshaambiwa mlango uko wazi”. Maneno hayo yalionekana kumuuma Kajala ambaye mara moja alikimbilia mabatini kituo cha polisi kwenda kumshtaki Harmonize kwa kitendo chake cha kuweka picha hiyo mtandaoni na kuleta tafsiri kuwa huenda wawili hao ni wapenzi kitu ambacho sio cha kweli, na yeye amepewa RB No/ KJN/ 73/2017 Jalada la uchunguzi

Kajala amesema;

“Nimemshtaki Harmonize ili ajue mimi sio mtu wa mchezo  kila wakati, maana ile video tulikuwa tukizungumza kawaida kwa nini aisambaze ili iweje kama sio kuchafuana huko”.

Kajala aliongeza kuwa anawashangaa wasanii wenzake Wolper na Wema kuingilia vitu kama hivyo kwa sababu wanaona kama yeye ni wakula mizoga yao. “Mimi nashangaa hivi wamenionaje, wanafikiri mimi ni wakula  mizoga yao nini wanayoiacha, wamenishangaza sana”.

Harmonize aliwasili kituoni hapo na kwa mujibu wa chanzo kinachoaminika kutoka kituoni hapo, Mwanamuziki huyo alijitetea kuwa sio yeye aliyeweka picha hizo mtandaoni bali ni mwanamke wake wa kizungu ndo aliyemtumia mtu mwingine kwa nia ya kutaka kumjua Kajala.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.