“Kama Diva Kataka Kuwa Single ni Maamuzi Yake” Heri Muziki

Mwanamuziki wa RnB ya Bongo fleva Heri Muziki amefunguka na kuongelea uhusiano wake na mtangazaji wa Clouds FM, Diva na kudai kuwa kama Diva ameamua kuwa single hayo ni maamuzi yake mwenyewe hawezi kumkataza.

Diva na Heri Muziki walianza mahusiano yao mwaka Jana na kuuweka wazi kwenye mitandao ya kijamii lakini wawili hawa wamekuwa wakitawala vichwa vya habari kuanzia wikiendi iliyopita baada ya kupishana kauli.

download latest music    

Ugomvi wao ulianzia studio za Clouds FM ambapo wawili hao walikuwa wanafanyiwa interview lakini kwenye maongezi walipishana baada ya Heri Muziki kufichua ukweli kwa kusema kuwa wawili hao hawako kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa sasa bali wapo pamoja kikazi jambo lililomkera Diva kwani alishasema Kuwa wao ni wapenzi.

Baada ya interview hiyi kuisha waliingia kwenye ugomvi mkubwa huku Diva akimtuhumu Heri kwa kumzalilisha baada ya kumkana redioni na baada ya hapo Diva aliingia Instagram na kusema kuwa yupo single akimaanisha ameachana na Heri Muziki.

Baada ya sakata hilo Heri amefanya interview na Millard Ayo na kufunguka yafuatayo:

Kabla ya kuingia kwenye interview tulifikia makubaliano kwamba sasahivi tubakie kama marafiki ili tufanye kazi Kwaiyo mahusiano kidogo tukaweka pembeni lakini sasa tumefika on air yeye anaongea hichi na Mimi naongea hichi lakini mpaka sahivi sijaelewa kwa nini anasema mimi  nimemdhalilisha kwasababu hata pale studio tulikubaliana yale niliyoyaongea lakini Kama ni maamuzi yake kuwa single sawa ila makubaliano yetu yalikuwa private”.

Lakini pia Heri amefunguka na kudai kuwa wanachopishana na Diva ni kuanika mambo yao binafsi kwenye mitandao ya kijamii kwani tangu mwanzoni mwa mahusiano yao alimwambia hataki yawe public lakini aliendelea akaenda kuyaweka public.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.