Kamwe Sitakaa Niusahau Mwaka 2018- Maua Sama

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Maua Sama aliyefanya vizuri na ngoma yake ya ‘Iokote’ amefunguka na kuweka wazi kuwa kamwe hatakaa asahau mwaka 2018.

Mwaka jana Maua Sama alijikuta katika wakati mgumu mara Baada ya kuwekwa mahabusu kwa muda wa siku 10 bila dhamana Baada ya kudaiwa kuidharau na kuichezea pesa.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Maua Sama amesema kuwa anaukaribisha Mwaka Mpya wa 2019 vizuri, lakini hatausahau 2018 kwani alipitia Mengi na kujifunza mengi.

Namshukuru sana Mungu nimemaliza mwaka salama japokuwa nimekutana na changamoto kubwa ambayo sikuitarajia kuipata ile ya kuwekwa ndani kutokana na ngoma hiyo ya Iokote.

Lakini nashukuru soo liliisha salama na nilijifunza ninatakiwa kuheshimu kila kitu, kwa hiyo sitarajii kitokee kitu kama kile tena katika maisha yangu.

Kwa sasa ninajikita zaidi kwenye kazi ya sanaa kwa kuwa najua nimejaliwa kipaji na nitatoa kazi ambazo wapenzi wa Maua wanahitaji ili niweze kukonga nyoyo zao”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.