Loading...

Karen Afungukia Mahusiano Ya Petit na Baba Yake Gadner

November 08, 2018 at 08:15
Karen Afungukia Mahusiano Ya Petit na Baba Yake Gadner

Msanii wa muziki kutoka THT anayefanya vizuri hivi sasa kwenye tasnia ya Bongo fleva na ngoma yake ya ‘Washa’ amesema Baba yake ambaye ni mtangazaji wa Clouds fm Gadner G Habash Hana tatizo na Petit Man.

Kwa wiki kadhaa kulikuwa na tetesi Kuwa Petit Man Ana mahusiano ya kiampenzi na Karen na hata kusemekana kuwa wamefunga ndoa Baada ya picha zilizowaonyesha wakiwa kwenye video shoot ya wimbo wake kusambaa mtandaoni.

Loading...

Katika mahojiano yake na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Karen amesema ingawa mitandao mingi ilikuwa ikiandika ndivyo sivyo kuwa yeye ana uhusiano wa kimapenzi na Petit Man, jambo ambalo si kweli Alisema familia yake inajua vizuri ishu hiyo kuwa ukaribu uliokuwepo kati yake na Petit na hata baba yake hakuwa na tatizo naye.

Watu wengi ninaojuana nao na baba anajuana nao vizuri kwa hiyo hata hiyo habari ilivyoanza kuvuma haikuleta shida kwa sababu familia yangu inafahamu kila kitu kuhusu Petit Man”.

 

Share

Comments

  1. Hayatuhusu

  2. Sasa juu inatusaidia aje

  3. Kwa raha zao

  4. Vyema tu

  5. Awesome

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment

Loading…