Karen-Sijapata Mwanaume Wa Kuwa Naye Kwenye Mahusiano

Msanii mchanga kabisa wa muziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri hivi sasa na ngoma yake ya ‘Washa’ Karen Gadner Habash amefunguka na kuweka wazi kuwa hana mpenzi kwa sababu hajapata mwanaume wa kuwa naye.

Karen alitengeneza headlines wiki chache zilizopita baada ya kusemekana kuwa kwenye mahusiano an kufunga ndoa na mume wa zamani wa Esma Platnumz, Petit Man Wakuache.

download latest music    

Karen amefunguka kuwa hana mahusiano na Petit Man kama ambavyo wengi walidhani bali ni marafiki tu na ni mtu ambaye aliamua kumsapoti kwenye kazi yake baada ya kuona wimbo ulihitaji kuwa na wanandoa.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5, Karen ameweka wazi kuwa hana mpenzi kwa sasa lakini endapo atatokea na katika muda sahihi basi atakuwa hana neno;

Kusema ukweli sina mpenzi kwa sasa nipo single lakini kama atajitokeza na kwa mtu ambaye nitakuwa namuhitaji basi nataka awe muelewa kuhusu kaiz yangu nzima ya usanii na aweze kunisapoti sana lakini pia aipende sana familia yangu hasa wazazi wangu kikubwa aweze kuwaheshimu”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.