Karl Lagerfield Afariki na Kumuachia Paka Wake Utajiri Wa Bilioni 456

Mbunifu maarufu wa mavazi  dunia Karl Lagerfield aliyefariki dunia siku mbili zilizopita ametajwa kuacha utajiri usiopungua Bilioni 456 na mrithi pekee anatajwa kuwa paka Wake anayeitwa Choupette.

Karl ambaye alikuwa mbunifu wa mavazi katika kampuni za Gucci na Fendi, alifariki Jumanne asubuhi, na Kifo chake kimeombolezwa na watu maarufu katika tasnia ya mavazi, ikiwa ni pamoja na dizaina wa Italia, Donatella Versace.

download latest music    

“Leo dunia imempoteza mtu maarufu,” alisema mhariri mkuu wa jarida la Vogue, Anna Wintour. Tovuti ya Lagerfeld inaonyesha alizaliwa mwaka 1938 japokuwa watu wengi wanasema alizaliwa miaka mitano kabla ya hapo.

Imeelezwa kuwa, Paka aitwae Choupette mwenye umri wa miaka Saba, aliyekuwa akimilikiwa na Karl Lagerfeld, ndiye anatazamiwa kurithi utajiri wa Mkongwe huyo anayetajwa kuwa na utajiri wa zaidi ya Tsh. Bilioni 456, Paka Choupette amekuwa akilelewa kifahari na Karl.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.