Khadija Kopa: Wasanii wa Taarab Wananiogopa

Msanii wa mziki wa miondoka ya taarabu ambaye anajulikana kama mslkia wa Taarabu nchini ameibuka na kudai kuwa wasanii wenzake wanamuogopa.

Mkongwe wa muziki huo wa taarabu amewachana wasanii wenzake wa taarabu na kudai kuwa wanamuogopa ndio maana hawawezi kutunga nyimbo zenye vijembe vinavyojibu nyimbo zake kama ilivyokuwa zamani, hivyo kawataka waache uoga wafanye wafanye ushindani ili taarabu iweze kufika mbali.

download latest music    

Khadija Kopa alifunguka hayo kwenye mahojiano aliyofanya na kituo cha televisheni cha East Africa ambapo alizidi kufunguka:

Mi naona kama wasanii waliopo wa taarabu ni kama wananiogopa wanaona mimi kama mama yao lakini vile vile hata kwa wao wenyewe wanatupiana madongo kuna nyimbo wanaimbiana lakini hawaendelezi alafu isitoshe sisi watu wa taarab wenyewe kwa wenyewe hatuna umoja yaani hatupendani kabisa yaani anaona nimuimbe fulani ili azidi kuwa staa sijui nsogopa kumpa kiki wakati mimi ni staa zaidi yake hivyo kunakuwa kuna kama wivu Fulani wakati mkifanya mashindano kama hayo ndo mnavutia mashabiki na wote mnajikuta mnapanda”.

Pia Khadija amesisitiza kuwa sio lazima kutafuta kiki kwa nguvu na zisizo za maana kama wasanii wengine wengi kama Bongo fleva bali ni kutumia ushindani wa kawaida wa kuimba ili kuzidi kukuza mziki huh wa taarab.

Hivi karibuni mziki wa Taarab umeonekana kupoteza ladha yake iliyokuwepo kama zamani na hata kupungua kwa mashabiki huku mashabiki wengi kudai taarab ilipoa baada ya Mzee Yusuphu kustaafu kufanya mziki huo.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.