Khadijah Kopa: Najutia Maamuzi Yangu Ya Kutoa Mimba Ujanani

Mwanamuziki wa taarabu nchini au wengi wanamjua kama Malkia wa muziki wa taarabu Khadijah Kopa amefunguka na kusema moja kati ya vitu anajutia maishani mwake ni kutoa mimba.

Kwenye mahojiano aliyokuwa anafanya na kipindi cha Kikaangoni cha East Africa Tv, Khadija Kopa amekiri ameshawahi kutoa mimba kadhaa na hata mimba nyingine kuharibika.

download latest music    

Ukishafanya kitu kama hicho lazima ujute, mambo hayo mambo makubwa hata Mwenyezi Mungu hayataki lakini ujana unakuwa unakutia wehu unashindwa kujua unakuja kujutia wakati huu.

Mimi najutia kutoa mimba ila nakumbuka wakati huo ndio nimesimama jina ndio limepemba moto halafu na ujauzito wapi na wapi lakini kila siku namuomba Mwenyezi Mungu anisamehe kwa sababu pengine huyo mwanangu angekuwa raisi? Lakini ni ujana maji ya moto na ninawambia vijana waliokuwepo wasifanye vitu hivyo”.

Lakini pia Khadija ameweka wazi kuwa anashukuru Mungu pamoja na mimba alizotoa alijaaliwa kupata watoto wengine wanne, ingawa alikataa kutaja idadi ya mimba alizotoa na aliweka wazi mimba zake nyingine mbili zilihariibika kwa bahati mbaya.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.