Kibenten Champonza Sista Fey Atimuliwa Kwenye Nyumba Ya Kupanga

Msanii wa Bongo fleva na bongo movie Faiza Omary  Maarufu kama Sista Fey amejikuta akitimuliwa Kwenye Nyumba aliyokuwa anaishi baada ya video na kibenten chake kusambaa mitandaoni.

Sista Fey na mpenzi wake Holly Star wamejizolea umaarufu Kwenye mitandao ya kijamii baada ya video zao kusambaa Lakini pia hilo limekuwa tatizo kwani wametimuliwa Kwenye Nyumba waliokuwa wanaishi.

download latest music    

Global Publishers wanaripoti kuwa Mwanzoni Fey hakuwa na kibenten wake huyo, lakini baada ya muda ndiyo akampeleka wakawa wanaishi wote ila mama mwenye nyumba alikuwa akikereka na maisha wanayoishi kwa kuwa kuna wakati wanabebana na kupelekana bafuni, jambo ambalo aliona siyo zuri kwa watoto wanaoishi kwenye nyumba hiyo.

Baada ya Tetesi hizo gazeti hilo lilimsaka Fey ili kutaka kujua ukweli wa jambo hilo ambapo alifunguka:

Unajua mimi ni mkweli sana, kwenye hilo siwezi kukataa, ni kweli nimepewa barua, lakini nimepokea kwa mikono miwili maana huyu (Eliasi) ndiye nimempenda. Mambo aliyoandika mama mwenye nyumba kwenye barua ni ya kawaida kwa wapenzi”.

Lakini pia Fey amesisitiza kuwa wana mpango wa kufunga ndoa na kibenten chake:

Baada ya kuzungumza na Sister Fey, Ijumaa Wikienda lilimgeukia jamaa huyo ili naye afunguke madai ya kumsababishia Fey kupewa barua ya kuhamishwa kwenye nyumba ambapo alisema yeye haoni kama kuna tatizo kwenye hilo ila inawezekana hapo hawakuwapenda tu”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.