Kidoa Amtetea Hamisa Mobeto Mitandaoni

November 14, 2017 at 11:59
Kidoa Amtetea Hamisa Mobeto Mitandaoni

Moja ya wauza nyago wanaofanya vizuri kwa sasa katika video za wasanii bongo  Ssha salumu mwenye jina la umaarufu kama Kidoa amefunguka na kumtetea mwanamitindo na video queen Hamisa Mobeto kwa wasanii wengine wa kike ambao wamekuwa wakimsema na kumsimanga kutokaa na nyingi  skendo   anazopitia hasa hili kubwa la kuzaa na msanii mkubwa Diamond Platinumz na mambo yote yanayoendelea kuhusu kesi iliyokuwa imepelekwa mahakamani kuhusu malezi ya mtoto huyo.

Mwanadada huyo anasema kuwa anakuwa anachukizwa na kuumiza na baadhi ya wasanii wenzie wa kike ambao kutwa kukaaa katika mitandao na kuwa wanamsema Hamisa bila kujua ni kitu gani mwenzao anapitia katika kipindi hiki kigumu na badala yake walitakiwa wamsaidia na kumpa sapoti ya ushauri na sio kumsema kila kukicha katika mitandao ya kijamii.

Loading...

Kidoa ambae alishinda taji la  Ijumaa Sexiest Girl kwa mwaka 2015 anasema kuwa kinachomshangaza ni jinsi wadada wamekuwa wakimsaidia Zari katika kumkandamiza Hamisa bila kujua kuwa maneno yao yanamwathiri mwanadada huyo kisaikolojia ukizingtia ni mbongo mwenzao.

Sio sawa wasanii wenzangu wanavyokaa wakimnyanyapaa hamisa hata kidogo, kutwa kumoiga vijembe wanatakiwa kukaa wakikumbuka kuwa hakuna ajuae kesha yake ,huenda  hata yeye mwenyewe hakuwaza kama yanaweza kumfika hayo yote. -Alisema Kidoa

Hamisa amekuwa ni moja ya wanadada gumzo katika mtandao kwa kipindi cha takribani miezi mitatu sasa tangu mtoto wake wa pili kuzaliwa na hii yote ni kutokana na kujulikana kwa baba wa mtoto kuwa ni wa Diamond Platinumz ambae tayari anafamilia nyingine yenye watoto wawili na Zari The Bossy Lady mwanamama tajiri kutoka Uganda.Hata hivyo Hamisa amekuwa akitajwa karibia kila kona katika mitandao huku wengine wakimkashifu kwa kujitegesha na kufanya makusudi kuzaa na msanii huyo ili aweze kupata pesa

5
Leave a Reply

avatar
5 Comment threads
0 Thread replies
0 Followers
 
Most reacted comment
Hottest comment thread
1 Comment authors
MercyMusaBridgetVictoriaCaroline Recent comment authors
newest oldest most voted
Caroline
Guest
Caroline

Fanyeni kazi bwana watu wasifanye mshindwe

Victoria
Guest
Victoria

Ni kweli kabisa

Bridget
Guest
Bridget

Tunakuelewa dada

Musa
Guest
Musa

Mambo ya mitandao ni udaku tu

Mercy
Guest
Mercy

Mtoto huyu huwaga mzuri sana


in Entertainment
Loading...

#Godseeker,
I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.