Kigogo Anayesimamia Bata Za Uwoya Aanikwa

Muigizaji wa Bongo movie Irene Uwoya amedaiwa kuishi maisha ya bata ndefu kwa sababu ya Kigogo mwenye pesa zake ambaye ndio mpenzi wa Uwoya kwa sasa.

Gazeti la ijumaa Wikienda linaripoti kuwa mtu wa karibu na Uwoya amepasua kuwa Uwoya anapewa jeuri ya pesa na  kigogo mzito aliyepo kwenye Serikali ya Kenya.

download latest music    

Ni kigogo (anamtaja jina, tunalihifadhi sababu hatujam­pata kuthibitisha) katika Seri­kali ya Kenya, ndiye ambaye anamuwezesha kwa kila kitu. Hizi sijui kufuru za bethidei yake, sijui kujiachia kwenye boti hadi Zanzibar kigogo huyo ndiye anayemuweze­sha”.

Chanzo hicho makini kilizidi kwenda mbali zaidi kwa kueleza kuwa, kutokana na uzito wa kigogo huyo, imekuwa ngumu kujulikana na hata anayejua pia huhofia kusema.

Ni kutokana tu na uzito wa kigogo huyo na bahati mbaya sana ni kwa sababu yupo Kenya, ingekuwa yupo Bongo ingekuwa ni rahisi sana watu kumjua.

Kigogo huyo ndiye anayed­hamini pia zile safari za mara kwa mara za Uwoya nchini Dubai, nafikiri huwa wanaku­tania huko na huyo kigogo kula zao raha.”

Baada ya tetesi hizo Gazeti hilo lilimsaka Uwoya ambaye alifunguka na kuweka wazi:

Hivi kwa nini kila mtu anapenda kumjua mtu wangu maana marafiki wanapenda kumjua, wasanii wenzangu, mpaka ndugu zangu yaani watu wa­nahangaika kweli jamani Lakini Huyo (anamtaja jina) nampenda sana labda niseme hivyo, siku akija Bon­go watu watafunga midomo yao”.

Uwoya alisisitiza kuwa hawezi kumtaka Mpenzi Wake kwa sasa Lakini muda ukifika atamuweka wazi.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.