Kiongozi wa Dini Ataka Kumbadilisha Alikiba na Chid Benz

Sheikh Abdulrazak ambaye ni maarufu kwenye mitandao ya kijamii, ameweka wazi mipango yake juu ya kumbadilisha msanii wa muziki wa kizazi kipya na kipenzi cha wengi, Ali Kiba, kumfanya amtumikie Mungu na kuachana kabisa na muziki wa bongo fleva.

Akiongea na Big Chawa kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Sheikh Abdulrazak amemtaja Alikiba na Chid Benz kuwa miongoni mwa wasanii anaokusudia kuwabadilisha imani yao, na kuachana na mambo ya dunia kama alivyofanikiwa kufanya hivyo kwa Mzee Yusuph na Sumalee.

download latest music    

“Chid Benz kwanza ataitwa Sheikh Rashid, chid benz hilo jina litapotea, target yetu sisi Chid Benz aje kuwa Sheikh Rashid, kama alivyo Sheikh Sumalee, kama alivyo Sheikh Mzee Yusuph, na kama atakavyokuwa Sheikh Alikiba na kadhalika, hizo ndio target zetu sisi”, amesema Sheikh Abdulrazak.

Ikumbukwe kwamba wasanii wawili aliowataja Sumalee na Mzee Yusuph, walikuwa ni wasanii maarufu na pendwa kwenye muziki wa bongo, lakini waliamua kuachana sanaa na kuanza kumtumikia Mungu.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.