Kisa Mama , Aslay Amliza Mama Yake Nandy.

Wikiendi hii inaweza kuwa ni wikiendi ya kihistoria katika swala la muziki , hii ni baada ya kufanyika kwa show kubwa iliyojulikana kama Aslay , Nandy na Marafiki huku lengo kubwa ikiwa ni kuwaburudisha wpenzi wa muziki hasa katika kusherekea siku ya wapendao  Ambayo ilifanyika February 17.

Akiwa anataka kutumbuiza wimbo wake unaokwenda kwa jina la mama, Aslay aliamua kumfuata mama na baba yake Nandy ambao pia walikuwepo katika show hiyo ili kuwakumbatia ikiwa ni kama ishara ya kuwaheshimu wazazi hao huku akiongea na kusema kuwa anatamani sana hata yeye mama yake angekuwepo katika show hiyo.

download latest music    

Huku akielekea katika meza hiyo, Aslay alikuwa akisema”kwa heshima kubwa napenda kwasimamaisha wazazi wa nandy ana nngependa wawe wazazi wangu pia, ninafuraha kuona wazazi wanawasapoti watoto wao,hsa mama na ninapomuona ninfarijika kwa sababu hata mimi nilitamani mama yangu angekuwpo hapa lakini hayupo.ninawaomna muwaheshimua sana wazazi hasa mama.

Hata alipokuwa akiimba wimbo huo watu wengi walionekana kuwa na huzuni kwa sababu ya msanii huyo kutoa lilipo moyoni mwake kuwa angetamani siku kama hiyo mama yake angeona mafanikio ya kazi yake kwa sababu walihangaika sana wote ili yeye awepale alipo.

Mama yake Aslay alifariki mnamo mwaka 2015, ambapo kwa histori aya maisha ya Aslay huwa anaumia sana anapokuwa akikumbuka au kuliongele atukio hilo kwa sababu mama yake alikuwa akimsaidia na kumfariji sana katika kufanya kazi lakini ilikuwa ni kama mshumaa uliozimika kwa sababu mama yake hajapata kuona mafanikio yake.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.