Kisa Ruge, Nandy na Msami Wamjia Juu Dudubaya

Wasanii Nandy na Msami wameoneshwa kukerwa na Dudubaya  baada ya Msanii huyo kutokuonyesha kujali hali ya mkurugenzi wa Clouds Media ambae wa sasa amekuwa mgonjwa sana na watu wamekuwa na  wakifanya kampeni ya kupata pesa kwa ajili ya  matibabu yake.

Msanii Dudubaya aliandika kuwa hakuna haja ya kujali kwa sababu hata yeye aliwahi  kuwadhurumu sana wasanii hivyo kwa sasa hivi Mungu yupo kwa ajili ya kumlipizia .

download latest music    

Alichosema Dudu baya kuhusu swala hilo

Hata hivyo wasanii wameonyeshwa kukerwa na maneno ya dudu baya akiwemo nandy pamoja na msanii kwa maneno hayo na waliamua kumjibu  :-

Alichojibu Nandy

Na baadae msami pia alikuja juu na kumtolea povu

“Bro Dudubaya unajua we ni rafiki yangu wa siku nyingi sana tangu sijaanza kuimba na umekuwa ukiniambia na kunishauri mengi sana tunapokutana… naomba na mimi leo pokea ushauri wangu……

Nikifatilia post zako nyingi sana naona neno MUNGU linatawala sana lakini sioni wewe ukiishi ndani ya hilo neno, umekuwa ukitumia maneno makali sana ambayo wakati mwengine sijui kama yanampendeza MUNGU wetu… mafundisho ya dini yanafunza kusamehe kwa kuwa tunafundishwa pia kuomba msamaa kwa MUNGU tunapokosea na tukijua kuwa MUNGU anasamehe….
Sina nia ya kwenda ndani sana lakini nakuomba “tafakari maneno yako, fananisha na imani ya MUNGU unayemtaja mara kwa mara” Zingatia Busara ya maneno pia”

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.