Loading...

Kisa Tanasha , Kim Atoa Povu Mahusiano ya Diamond

January 11, 2019 at 04:29
Kisa Tanasha , Kim Atoa Povu  Mahusiano ya Diamond

MREMBO ambaye anadaiwa kumwagwa na mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Lilian Kessy ‘Kim Nana’ ameibuka na kulitolea povu penzi jipya la msanii huyo na mrembo kutoka Kenya, Tanasha Donna ’.

Kim ametoa povu hilo hivi karibuni mara baada ya Amani kumtaka azungumzie penzi jipya la Diamond ambaye awali iliaminika kuwa ndiye mumewe mtarajiwa kabla jamaa huyo hajaibuka na Tanasha.

Loading...

Akimzungumzia zilipendwa wake huyo, Kim alisema mambo ya Diamond na Tanasha hayamhusu huku akielekeza lawama zote kwa mitandao ya kijamii.

Hivi mnajua kiasi gani nimetukanwa kwenye mitandao ya kijamii? Na pia watu wa mitandao hawajui kabisa kufuatilia vitu kwa kina wanachojua ni kutukana watu lakini nashangazwa sana mimi kuhusishwa na Diamond, naomba kuweka wazi leo siko kwenye mapenzi na Diamond kwa sasa mimi nina maisha yangu na yeye hivyohivyo ndiyo maana amemuweka wazi mpenzi wake mpya kama ningekuwa ni mimi si angewaambia mashabiki zake kuwa ni mimi?” .

Baada ya kumwaga povu hilo, Amani lilimbana zaidi kuhusiana na ishu ya kubadilishwa dini na mama Diamond ambayo iliwahi kuripotiwa na gazeti hili mwishoni mwa mwaka jana.

Unajua hiyo ni sawa lakini siwezi kuwa na jibu la moja kwa moja kwenye hilo kwa sababu anayeweza kuzungumza vizuri ni mama Diamond mwenyewe.”

Hata hivyo Amani lilijaribu kumvutia waya mama Diamond, Sanura Kassim ‘Bi Sandra’ lakini simu yake iliita muda mrefu bila kupokelewa

Share

Comments

  1. hahahaha

  2. michepuko imekasirika

  3. yataka galby tena sana

  4. Mami pambana na hali yako

  5. nacheka maanake Mondi hakuwai kutambulisha aliyekua akiongea kila siku ni huyo bi sandra sa sijui ndiye aliyekuoa au vipi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment

Loading…