Kivazi Cha Kitenge Kinavyowatoa Wanaume

October 12, 2017 at 12:26
Kivazi Cha Kitenge Kinavyowatoa Wanaume

Ilishazoeleka kuwa vazi la kitenge ni maarufu kwa wakinamama na wakina dada tu, lakini siku hizi mambo yamebadilikakabisa , mishono n mitindo imezidi kuwa mingi, fashion inazidi kupanuka na wanaume nao wameamua kuja na fashion ya vitenge tena imekuwa ikiwatoa isivyo kawaida.hawa ni baaadhi ya wasanii wa Tanzania wa kiume walitokea vizuri kabisa katika kivazi cha kitenge.Raha ya kivazi hiki ni kwamba hakichagui wapi pa kuvaa, unaweza kuvaa kanisani, ofisini na hata katika mitoko mbalimbali.

 

Hemed phd ni mmoja wa wasnii wa bongo fleva, yeye amekuwa mstari wa mbela kabisa katika mavazi ya kitenge, hata katika nyimbo yake mpya amuamua kutoka na kitenge, sio lazima ushone shati tu , hata suruali pia, lakini hata ukivaa full bado unaonekana maridadi.

Diamond Platinumz hivi juzi alituwakilisha vyema kama huku nchi za ulaya alipoenda kuchukua tuzo yake, lakini hakusita kuvaa kivazi cha kitenge ambacho kilimtoa vizuri kabisa, alafu chini akatupia raba kali kabisa.

Mabeste, akiwa ametoka vizuri kabisa na kivazi cha kitenge , aina ya makenzi.vitenge hivi vinapendwa sana hasa kwa wanaume wakivaa mashati

Quick rocka , nae aliamua kutupia kivazi cha kitenge murua kabisa na suruali yake nyeusi .Raha ya kitenge kinakufanya unaonekana maridadi kabisa na umaweza kuvaa sehemu yoyote.

Fahad Fuad ni moja ya wanamitindo maarufu na video model anaefanya vizuri Tanzania akiwa ametupia kivazi chake  cha shati kilichochanganya na  kitenge maridadi kabisa.

Kitu kingine kinachovutia kwenye kitenge ni kwamba sio lazima uvae kitenge chote, msanii Ben Pol aliamua ku-design shati lake akaweka nakshi za kitenge mikononi na baadhi tu ya sehemu na bado aalionekana maridadi kabisa.

 

Leave a Reply

5 Comments on "Kivazi Cha Kitenge Kinavyowatoa Wanaume"

avatar
newest oldest most voted
Kingsley
Guest
Kingsley

Mavazi yametulia poa sana

Juma
Guest
Juma

Wamependeza wote

Happiness
Guest
Happiness

Maridadi fashion hii inamfanya mtu kuwa smart balaa

Gabriela
Guest
Gabriela

Kitenge ndo habari za mjini kwa sasa

Mohamed
Guest
Mohamed

Mimi nazipenda sana maana natokea mwafrika kamili


in Fashion
Loading...
wavatar

#Godseeker,
I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.