Loading...

Kujiamini na Kusimamia Ninachokiamini Kimenipa Mafanikio-Rosa Ree

August 09, 2018 at 08:46
Kujiamini na Kusimamia Ninachokiamini Kimenipa Mafanikio-Rosa Ree

MSanii wa Muziki wa Bongo fleva anayetamba kwa miondoko yake ya kipekee ya kurap amefunguka na kutoa siri yake iliyompa mafanikio mpaka leo yupo alipo kama Mwanamuziki.

Rosa Ree ambaye amewahi kufanya vizuri sana na wimbo wake ‘Way Up’ amefunguka na kuweka wazi siri ya mafanikio yake kwanza ni kujiamini halafu na kuamini anachokifanya.

Loading...

Kwenye mahojiano na  Global Publishers, Rosa Ree alifunguka kuwa muda mwingi huko nyuma watu walikuwa wanamwambia kwamba anajifanya mnyamwezi kwa soko la Bongo hawezi kufika popote, lakini hakuwasikiliza kwa sababu alikuwa anawaza kwenda kimataifa.

Nisingejiamini na kusimamia kile nilichokiamini kiukweli nisingefika mahali nilipo leo, siku zote nilikuwa ninatazama soko la kimataifa, kwa hiyo hata maneno ya kunikatisha tamaa sikupenda kabisa kuyapa nafasi”.

Rosa Ree alizidi kupata mafanikio hivi karibuni baada ya kusaini dili la mamilioni na Recording Label  kutoka Afrika ya kusini ambayo ilimpatia nyumba mbili za kifahari.

Share

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment

Loading…