Lady Jay Dee Aikataa Rockstar 4000 ya Alikiba

Baada ya kusambaa kwa  taarifa za Lady Jay Dee kujitoa kwenye Label kubwa Africa ya Rockstar 4000 imbayo pia inawasimamia Ali Kiba na Ommy Dimpoz mapya yaibuka.

Akiongea na Bongo 5 mtu wa karibu wa msanii huyo amedai, Jide hajawahi kusaini mkataba na label hiyo kwa maana hakuna picha zilizowahi kuonyesha mkataba  huo, alikuwa anafanya kazi na Seven Mosha ambaye ni boss wa label hiyo Kama rafiki yake wa muda mrefu aliyekuwa anamsaidia kazi katika mziki wake.

download latest music    

“Nafikiri kaamua kaacha tu kufanya kazi na Seven. wewe mwenyewe unaona wasanii Wa Rockstar au WCB au hats artist yoyote anaposaini mkataba huwa anaonyeshwa kwenye media au huwa anatangazwa kabisa Kuwa ni msanii wao. Kwa Jay Dee hicho kilikuwa hakijafanyika ni kwamba wao walikuwa wanafanya kazi tu na  Seven na sio directly na Rockstar, Pua ilikuwa ni process wanapima Kama baadae Jide ataingia Rockstar lakini nafikiria hawakufika muafaka huo.

Chanzo hicho kiliendelea kueleza:

“Kama kulikuwa na kitu cha Jay Dee ambacho angeweza kukipush alifanya hivyo kwa sababu tu Seven na Jay Dee n marafiki wa siku nyingi”.

Hata hivyo mtu huyo amesisitiza kuwa hakuna ugomvi wala tatizo lolote lililopo kati ya Seven na Jay Dee kwani urafiki wao bado upo pale pale kama ilivyokuwa zamani.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.