Lady Jay dee , Juliana Kanyomozi Kuwafikia Mashabiki October 2018

Mwanadada  mwenye heshima zake katika sanaa ya bongo fleva Judith Wambura maarufu kama Lady jay dee ametangaza ujio wake mpya na msanii mwingine mkongwe kabisa na mataalamu wa muziki kutoka Uganda mwanadada Juliana Kanyomozi mwaka huu .

Akiandika katika ukurasa wake wa instagram, Lady jay dee aliweka picha yake na mwanadada Juliana na kuandika maneno yanayoashiria kuwa kuna kitu wanataka kufanya na kuweka verification ya muda kuwa itakuwa ni mwaka 2018 October.

download latest music    

Lady jay dee  na Juliana wanaweza kusemwa kuwa na historia moja ya muziki ingawa kila mmoja ana nafasi yake katika nchi yake , hii ni kutokana na ukubwa wao katika muziki lakini pia wamekuwa wasanii wa  muda mrefu na wamekuwa wasaidizi na mfano kwa kuigwa wa wasanii wachanga wanaoingia katika game la muziki.

Hata hivyo chochote wanacghotaka kufanya wasanii hawa kinaaminika kuwa na manfaa kwa nchi zote mbili na kwa muziki wa nchi zote lakini kubwa zaidi ni burudani nzuri kwa mashabiki.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.