Lady Jay Dee na Gadner Uso Kwe Uso Msibani

Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Judith Wambura maarufu kama Lady Jay Dee amekutana uso kwa Uso na aliyekuwa mume wake mtangazaji Gardner G Habash katika msiba wa mke wa Kibonde siku ya jana.

Lady Jay Dee na Gadner walikuwa wanandoa kwa miaka kama kumi kabla ya kuachana na kupeana miaka michache iliyopita kwa sababu zisizojulikana kwa watu wengi.

download latest music    

Lakini baada ya wawili hao kuachana kulitokea bonge la bifu baina yao hadi kufikia hatua ya Gadner kumwagia Matusi Lady JD hali iliyopelekea kupelekana mahakamani.

Lakini baada ya talaka kutoka Lady jay Dee alitangaza Kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa hana bifu kabisa na Gardner na kuomba kila mtu aendelee na maisha yake.

Siku ya jana wawili hao walikutana Uso kwa Uso huku Lady JD akiwa na mpenzi wake mpya Spicy Muziki Wote wawili walipeana mikono na kisha kumfariji mfiwa.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.