Lady JD Ataja Kitu Kinachoua Muziki Wa Bongo Fleva

Msanii Mkongwe wa muziki wa Bongo fleva nchini Judith Wambura maarufu kama Lady Jay Dee amefunguka na kuweka wazi kitu ambacho kimekuwa kikiua muziki wa Bongo fleva.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kituo cha habari, Lady Jay Dee ameitaja mitandao ya kijamii kama kitu kinachoua muziki wa Bongo fleva kulinganisha na miaka ya nyuma Wakati mitandao haikuwepo:

download latest music    

Kitu kimoja ambacho nimeangalia ambacho kinaharibu tasnia ni kufikiri kwamba kuangaliwa YouTube ndio kufanya vizuri kwenye kiwanda cha sanaa, YouTube sio kipimbo cha wimbo kuwa mzuri au kufanikiwa.

kwa sababu kuna vitu vingi sana mtandaoni, kuna mtu anaweza kuwa anaenda kuangalia ni nini”.

Kwa sasa Lady Jaydee yupo kwenye maandalizi ya mwisho ya show yake ya Vocals Night itakayofanyika October 28, 2018 kwenye ukumbi wa Mlimani City.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.