Lady JD Kuwapa Shavu Wabunifu Wa Mavazi na Mitindo

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Judith Wambura maarufu kama Lady jay Dee ametoa fursa kwa wabunifu wa mavazi na wanamitindo atakaowatumia kwenye video ya wimbo wake mpya.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Lady Jay Dee ametangaza kuanza kuchukua maombi ya watu ambao atawatumia kwenye kazi yake:

download latest music    

Nita shoot video yangu ya kwanza kwa mwaka 2019 nchini Afrika ya Kusini siku ya Alhamis 10th January 2019. Nakaribisha Stylists wapya wa nguo, Jewelry, Viatu n.k kwa siku ya leo na kesho tu,”

Lakini ni pia Jay Dee ameweka wazi masharti ya watu atakaoweza kufanya nao kazi:

Unaweza kuniandikia email na kutuma picha ya vitu unavyotaka vionekane, au kutuma kwa WhatsApp kwenye number iliyopo kwenye profile yangu. Zingatia uafrika zaidi katika designs utakazotuma na u modern kidogo ukiwemo sio mbaya“.

https://www.instagram.com/p/BsXjejBB2tS/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=15912avzwe84t

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.