Linah Aongelea Mimba Ya Mtoto Wake Wa Pili

Msanii wa Bongo Fleva ambae amekuwa kimya kwa muda kidogo kutokana majukumu ya kujifungua na kulea, EsterLinah Sanga amefunguka na kusimulia jinsi mimba  ya mtoto wake wa pili itakavyokuwa. Linah ambae alifanya arobaini ya mtoto wake wa kike anaejulikana kama Tracy Paris kama wiki mbili zilizopita amesema kuwa yeye hana mpango wa kuzaa watoto wengi bali watoto wawili tu huyo wa kwanza na ataongeza wa pili atakayekuwa wa mwisho.”Niko na mpango wa kupata watoto wawili tu , huyu wa kwanza na wapili atakuwa wa mwisho , sikuwa na  plan za kupata watoto wengi kabisa”alisema Linah

Hata hivyo katika mahojiano hayo na kituo cha Televisheni cha Eatv, Linah aliulizwa kuhisu kupiga picha kama alizopiga katika mimba yake ya kwanza “siwezi kujua,mimba itakavyokuja itanipeleka vipi maana kila mimba ina mambo yake, itategemea na muda pia,ila mimi ni msanii siwezi kuficha maana ntaenda hapa na pale , ntajulikana tu, picha ntapiga” alisema

download latest music    

Alipoulizwa kama kelele za mara ya kwanza zinaweza kumzuia linah kupiga picha kama zile za mwanzo linah anajibu kuwa “kelele zile hazikuniboa,kwa sababu hata nikifanya kitu kizuri kuna watu watapenda na watu wengine wataponda tu huwezi kumridhisha kila mtu,, ukipiga picha na gauni refu watakwambia mshamba, likiwa fupi watakwambia gauni fupi”

Hivi karibuni kunakuwa na tabia ya watu kupiga picha za ujauzito huku wakiacha miili yao yote nje, ambapo haikuwa tamaduni za kitanzania lakini kwasababu wanasema wanakwenda na wakati imekuwa kawaida kwao, Linah ni mmoja wa wasanii ambao walipiga picha za ujauzito akiwa ameacha wazi badhi ya maungo yako , na baadhi ya mashabiki walimtupia maneno katika mitandao kuhusu picha hizo.Kwa Linah anasema hakukerwa kabisa na kelele hizo

Linah anaendelea kuelezea kuwa kuna baadhi ya watu walikuwa wakisema amechelewa kujifungua, ila yeye mwenyewe anasema hakuchelewa kujifungua bali watu walijua mapema kuhusu ujauzito wake, alikuwa na mimba ya miezi mitatu watu wakawa tayari wamejua lakini alijifungua mimba ikiwa na wiki 36 na siku 5 ivyo huwa ni kawaida kwa baadhi ya watu ila tu alikuwa na tumbo kubwa.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.