Linah: Sikupanga Kuwa na Mtoto Kipindi Hiki

Msanii wa Bongo fleva, Linah Sanga amefunguka na kudai hakuwa amejipanga kuwa na mtoto kwa kipindi hiki lakini anamuomba Mungu isiwe kigezo cha yeye kupotea kimuziki ili aje kuwa mfano kwa wasanii wenzake wa kike wanaogopa kubeba ujauzito.

Linah amebainisha hayo katika mahojiano aliyofanya na EATV hivi karibuni, Baada ya kuwepo imani kwa baadhi ya watu kudai kuwa msanii akioa, au kuolewa au hata kupata mtoto anakuwa hawezi kuendelea kufanya vizuri katika kazi yake kutokana na majukumu ya ulezi yanaongezeka na kupelekea kupotea katika industry ya muziki.

download latest music    

“Namuomba Mungu usiku na mchana nisije kupotea katika gemu sababu ya uzazi ili iwe mfano hats kwa wengine ambao watakuja nyuma yangu, labda wanaogopa kuzaa kwa kufikiri watapotea, Ila mi nahisi ni mtu tu anavyoishi na mashabiki zake”.

Pamoja na hayo Linah ameendelea kwa kusema;

“Sikuwa nimejipanga kupata mtoto katika kipindi hiki ila nilikuwa na-wish nipate ujauzito nizae lakini sikufahamu ni lini itatokea hivyo. So kipindi kile nilichokuwa na-wish nilhataa kila nikijaribu haingii, nikajisahau nikajikuta imekuja hats sijatarajia lakini kwa Kuwait nilikuwa na uhitaji nikasema haina neno. Japo nilishauriwa vitu vingi mwanzoni lakini nikasema hapana kwa kuwa nimetaka kuzaa acha nifanye hivyo”.

Linah kwa upande mwingine amesema anajipa mapumziko katika kufanya kazi sake nakuwasihi mashabiki zake wamvumilie mpaka mwakani (2018) mwanzoni ndipo atakapoachia kazi yake mpya.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.