Linex Afunguka Kutomuona Mtoto Wake Kwa Miaka Minne

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Sunday Sangu maarufu kama Linex ‘Sunday Mjeda’ amefunguka na kuweka wazi kuwa mzazi mwenzake amempora Mtoto Wake.

Linex ameeleza kisa cha mwanamke ambaye alikuwa Mpenzi Wake na kuzaa naye kumgeuka na kumchukua Mtoto wao ambaye hajamuona kwa miaka kadhaa sasa.

download latest music    

Katika mazungumzo na Gazeti la Ijumaa Wikienda , Linex alisema kuwa hajamuona mtoto wake huyo wa kiume takribani miaka minne iliyopita tangu aliponyang’anywa nyumbani kwa mama yake.

Yaani kinachoniuma mtoto wangu ana miaka 12 sasa, najua angekuwa na furaha sana ya kuwa na mimi lakini mpaka sasa sijui alipo wala pakumpata maana mama yake mpaka simu kabadilisha nasikia tu anaishi Kahama, nina hamu sana na mwanangu”.

Inadaiwa sakata hilo lilitokea Baada ya Linex na mzazi mwenzake kuvurugana ndipo mwanamke huyo alibeba kilicho chake na kuondoka na Mtoto wao.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.