Lulu Diva Adai Hakuna Mwanaume Kama Idris

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Lulu Abbas maauru kama Lulu Diva ameibuka na kumwagia sifa kibao msanii wa sanaa ya vichekesho Idris Sultan na kudai kuwa hakuna mwanaume kama Idris Sultan.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Lulu Diva aliandika kuwa hakuna mwanaume mzuri kama Mshindi wa Big Brother 2014, Idris Sultan.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Lulu Diva alitakiwa afafanue kwanini ameamua kumwagia sifa hizo Idris  alisisitiza kwamba, ameamua kuandika maneno hayo kwa sababu kaka yake huyo ni handsome (mzuri) na uzuri wake hauwezi kuufananisha na mwanaume mwingine yeyote Bongo.

Ndio ni kweli nimeandika hivyo kwenye akaunti yangu ya Instagram kwa sababu Idris ni handsome jamani kwani we huoni? Halafu kila siku mi’ huwa namw-ambia hata tukio-nana sema nikaona haamini ndio maana nikaposti kuonesha msisitizo”.

Lulu Diva aliweka wazi kuwa yeye na Idris ni ndugu kwa maana kuwa ni Mtoto wa mama mdogo na mama mkubwa

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.