Lulu Diva akatwa Kutumbuiza Fiesta Grand Finale

Msanii lulu Diva amesonyesha kilio chake kwa kuililia serikali iwafikilie wasanii ambao wataondlewa katika Fiesta ya mwisho itakayo fanyika jijini Ea es Salam mwaka huuu ikiwa ni kullele cha tamasha ilo ambapo kwa tamko la serikali tamasha ilo litapaswa kuisha saa sita usiku.

Akiongea na vyombo vya habari, mkurugenzi wa uzalishaji wa vipindi Clouds Media  Bw.Ruge Mutahaba alisema kuwa kwa ratiba hiyo ni lazima wapunguze idadi ya wasanii  watakao perfom siku iyo ili kuweza ku-balance muda unaotakiwa. Lakini bado alitoa tumaini kuwa kuna uwezekana wa kupata kibali cha kupitisha mud na ikitokea kibali kikapatikana basi wataweza  kuweka wasanii wote waliopangwa.

download latest music    

Lulu Diva ni mmoja wa wasanii ambao walokuwa wakinufaika na tamsha hilo kwa sababu kwanza ndio mara yake ya kwanza  kufanya show katika tamsha ilo amabpo alipata bahati  ya kutumbuiza katika baadhi ya mikoa iliyopita hapo awali lakini kwa sasa amethibitisha kuwa kutokana na mabadiliko hayo ya ratiba yeye pia ni mmoja wa wasaniiwaliokatwa kutumbuiza katika show hiyo kubwa ambayo kwake ingekuwa ni ‘dream comes true’ kwa kuifanya kwa mara ya kwanza kwenye mkoa mkubwa wa jijini Dar Es Salam.

Lulu Diva ambae mwanzoni alikuwepo katika orodha hiyo,  lakini baada ya tamko ilo alipokea ujumbe kuwa ameondolewa katika orodha kutokana na tamko la mkuu wa mkoa.Hata hivyo Lulu Diva anaiomba serikali kuwafikilia kwa sababu  kulipwa kwake kunategema watu wengine wengi nyuma yake na ukizingatia kuwa kwake ilikuwa ni kama ndoto kufanya show katika jukwaa kubwa kama hilo.

mwaka huu ndio mwaka niliotimiza ndoto yangu kwa  kutumbuiza kwa mara ya kwanza katika jukwaa la fiesta, ujira wangu  ninaoupata pale ninagawana na watu wengi sana nyuma yangu  kuna dereva, kuna make-up artist, na wengine wengi sana ndio maana ninaiomba serikali itufikilie sana sisi wasanii. Alifunguka Lulu  Diva

Tamasha la fiesta linategemea kufanyika tarehe 25 novemba katika viwanja vya leaders club na baadhi ya wasanii ambao mpaka sasa wapo katika orodha ni pamoja na Alikiba, Vannesa mdee, Madee, Fid Q, Weusi, Nandy, Ben Pol.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.