Lulu Diva Awaeleza Mashabiki wake Siri ya Urembo Wake

Mwanamuziki mrembo wa Bongo fleva Lulu Diva ameamua kuwapa mashabiki zake siri ya weupe wake, Lulu alifika hatua hiyo baada ya watu wengi kuingiwa na kasumba kuwa wasaani wengi wa kike au hata wa kiume wana tabia ya kujichubua na kuwa weupe.

Katika mahojiano wengi aliyoyafanya na East Africa radio katika kipindi chao cha Planet Bongo Lulu amekiri kuwa siri kubwa ya urembo wake na weue wake unaofanya kuwa mrembo ni kula matunda na mboga mboga.

download latest music    

Lulu alisema;

“Msanii unatakiwa kuanza kujibrand kuanzia mwili wako, ngozi yako, vitu unavyokula, naweza sema kuwa nakula sana mboga mboga na matunda na kuna baadhi ya vyakula vinasaidia ngozi kung’ara”.

Luu Diva ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake unaoitwa  ‘Give it to me’ ameamua kuweka wazi swala hilo kwani watu wengi wamekuwa wakiwashutuma wasanii kwa kutumia mikorogo ili wawe weupe kwa kuamini kuwa ndio wanakuwa warembo zaidi.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.