Lulu Diva Kujiweka Kando na Mitandao Ya Kijamii

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Lulu Abbas maarufu kama Lulu Diva ameibuka na kuweka wazi kuwa Hivi sasa hana mpango wa kuweka mambo yake kwenye Mitandao ya kijamii.

Lulu Diva ambaye siku za nyuma aliwahi kuanika Mali zake kama gari, Nyumba na vinginevyo ametangaza kujiweka kando na mitandao ya kijamii ili kuishi maisha yenye uhalisia wake.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Dimba, Lulu Diva amesema kuwa wasanii wengi wanaishi maisha ya uongo mitandaoni kuliko uhalisia wao kitu ambacho kwake ameamua kujiweka nacho kando.

Nilichojifunza wengi wetu tunapenda kudanganywa, mtu anataka kuona unaonyesha maisha feki mitandaoni ndio akufuatilie, mfano mimi kwa sasa sipost mambo yangu lakini watu wananiandama kwamba nimefulia, hii inafurahisha sana”.

Hata hivyo Lulu Diva amekana vikali Tetesi Za kuwa amefulia kutokana na watu kutomuona akianika maisha yake kwenye Mitandao ya kijamii kama ilivyokuwa zamani.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.