LuLu Michael Akiri Kunyooshwa Na Zari

Haikuwa matarajio ya wengi kuwa Zari The Bossy akifika Tanzania ataweza kupokelewa kwa shangwe kama ilivyokuwa mwanzao.Hii yote ni kutokana na mambo mengi mengi yaliyotokea hapo katikati,  baada ya marumbano na scandal nyingi zilizokuwa zikiiumba familia ya Diamond na mama mzazi  wa watoto wake (Zari) , watu wengi katika mitandao walikuwa wakionyesha kuwa na chuki na Zari The Bossy malkia kutoka Uganda.

Lakini weekend hii Zari The Bossy alikuaja Tanzania kwa ajili ya kufanya uzinduzi wa duka lingine kubwa la Mlimani City mali ya Gsm,akiwa kama balozi Zari alitakiwa kuonekana kwenye uzinduzi wa duka ilo ivyo ilibidi yeye kuja Tanzania.Kitu cha kushangaza au cha kufurahisha ni jinsi ambavyo Mama Tee alivyopokelewa kuanzia uwanja wa taifa mpaka katika shughuli hiyo, watanzania walikuwa mstari wa mbele kumshangilia sana .

download latest music    

Kutoka kwa malkia wa bongo movie, Elizabeth Michael nae hakusita kuonyesha hisia zake kwa tukio ilo la watanzania kujaza umati katika viwanja vya Mlimani City katika uzinduzi huo ambao Zari pia alikuwepo, na inawezekana kabisa umati huo ulijazwa na uwepo wa Zari katika uwanjan huo.kitu ambacho ni mara chache kutokea kwa wasanii wa Bongo wenyewe.

Katika ukurasa wake instagram, Lulu Michael aliandika”Ule umati wa Mlimani City leo wa kumuona Mama Tee….Dada ametunyoosha nyumbani kwetu wenyewe.TUMPENDE Tu..HATUNA NAMNA” aliandika Lulu

Inaweza kuwa ni kama fundisho kwa wasanii wengine wakaubwa Tanzania kuwa Zari The Bossy , amekuwa ni mwanamke aliyeweza kujizolea mashabiki kibao kiasi kwamba wanatokea kumsapoti kuliko hata ambavyo  wanavyokuwa wanasapotiwa wasanii wenyeji, swali la kujiuliza ni kuwa je Zari ana nini na watanzania, Zari amewafanyia nini watu hawa mpaka kufikia hatua ya kumsapoti kiasi icho.Nadhani mashabiki wanasapoti pale ambapo wanaona mtu yuko makini na kile anachokifanya.

Zari ni mwanamke wa msanii mkubwa Tanzania , kumekuwa na mambo mengi na ugomvi hapo katikati, watanzania walidhaniwa kuwa ndo watu wa kwanza kumchukia mwanamama huyu lakini nadhani kutokana pia na jinsi Zari amekuwa aki-handle matatizo ya familia yake vizuri  na kujitahidi kuwa-keep mashabiki wake ndicho kitu kinachowafanya watu wazidi kumkubali zaidi.hivyo wasanii waache kusema huyu wa huku au kule wanapaswa kuiga kitu kutoka kwa Zari , ambae nadhani yupo makini sana na kazi, biashara na mashabiki wake wanaomfanya aendelee kufanya vizuri katika kazi zake.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.