Lynn Adaiwa Kutimuliwa Kwenye Mjengo Aliokuwa Anaishi

Video vixen na msanii wa Bongo fleva Irene Louis maarifu kama Official Lynn amejikuta katika wakati mgumu baada ya taarifa kuenea kwenye Mitandao ya kijamii kuwa ametimuliwa kwenye mjengo aliokuwa anajiachia nao.

Miezi michache iliyopita Lynn ambaye amewahi kuwa kwenye mahusiano na Diamond Platnumz alizua gumzo Baada ya kuanika Mali zake kwenye Mitandao ya kijamii ikiwemo mjumba wa kifahari ambao alidai ni Mali yake.

download latest music    

Lakini mambo yamesemekana kumuendea kombo mrembo huyo kwani mjengo huo umeonekana kwenye page ya Dalali na kwa Jinsi inavyoonekana Nyumba ile ilikuwa ya kupangisha tu.

Dalali huyo ameweka wazi kuwa mjengo huo utakuwa wazi kuanzia mwezi wa tatu Baada ya mtu anayeishi hapo Hivi sasa (ambaye ni Lynn) kutegemewa kuhama.

Habari za kimbea mtandaoni zinasema kuwa mrembo huyo amemwagana pedeshee ambalo lilikuwa linasimamia shoo na hivyo kusababisha Kufulia.

Lynn ambaye Hivi sasa anafanya muziki wa Bongo fleva na anafanya vizuri na ngoma yake ya ‘Chafu’ hajasema chochote kuhusu sakata hilo Mpaka Hivi sasa.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.