Lynn Akiri Kutamani Ndoa Katika Umri Wa Miaka 19

Muuza nyago maarufu katika video za wasanii mbali mbali Irene Godfrey maarufu kwenye social media Kama Official Lynn amefunguka na kudai anatamani sana ndoa hata Kama ana umri wa miaka kumi na Tisa tu.

Kwenye interview yake na Gazeti la Ijumaa, Lyyn aliyewahi kudaiwa kutoka kimapenzi na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ alisema kwamba japokuwa ndoa ni mipango ya Mungu lakini yeye anatamani sana kuolewa na kutulia katika ndoa yake kwa sababu itamuepusha na mengi ambayo anazushiwa sasa.

download latest music    

Unajua zamani malengo yangu yalikuwa kuolewa nikiwa na umri wa miaka 26 lakini kila siku zinavyozidi kwenda ndio nazidi kutamani ndoa kwa kweli sijui kwa sababu mtu wangu ananijali sana na kunipa mapenzi ya kweli, ingawa sitakuja kuweka mahusiano yangu wazi kwa sababu bebi wangu hapendi labda mtakuja kumjua tukioana“.

Lakini pia Lynn amejitapa kuwa Bongo yeye pekee ndiye staa ambaye anamiliki vitu Bongo vya thalami katika umri mdogo Kama vile Magari manne ya kifahari na Nyumba mbili.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.