Lynn Akiri Kuwahi Kuwa na Tabia Ya Udokozi

Video vixen maarufu ambaye sasa ni Msanii wa Bongo fleva Irene Godfrey Louis maarufu kama Lynn amefunguka na kuweka wazi kuwa aliwahi kuwa na tabia ya udokozi.

Mrembo huyo ambaye amewahi kuwa Mpenzi wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, ametoa siri  jinsi alivyokuwa anapen­da kula maziwa ya unga kiasi kwamba alikuwa anadiriki kudokoa pesa za mama yake ili mradi tu akanunue maziwa hayo.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la  Ijumaa Wikienda, Lynn al­isema alipokuwa mdogo alikuwa anapenda sana kulamba maziwa ya unga, ikawa asipoyapata ana­kosa amani hivyo alifanya kila awezalo apate pesa akayanunue.

“Yaani nilikuwa napen­da sana kulamba maziwa ya unga kiasi kwamba nilianza kuwa na katabia ka’ kudokoa pesa za mama ilimradi tu ni­pate maziwa ila ikafika wakati mama ikambidi azoee hiyo hali, akawa ananipa pesa nika­nunue ili nisizoee tabia ya wizi”.

Lynn Alipay’s umaarufu Baada ya kuwa video queen kwenye wimbo wa Rayvanny ‘Kwetu’ na Hivi karibuni ametoa wimbo wa kwanza na kutangaza rasmi kuingia kwenye muziki.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.