Lynn Awatolea Povu Watu Wanaohoji Utajiri Alionao

Video vixen maarufu katika tasnia ya Bongo fleva Irene Jeffrey Louis maarufu kama Lynn amefunguka na kuwatolea povu zito watu ambao wamekuwa wakihoji utajiri ambao amekuwa akijionyesha nao Kwenye mitandao ya kijamii.

download latest music    

 

Wiki iliyopita Lynn aliweka wazi kuwa pamoja na kuwa mdogo mwenye umri wa miaka 18 tu lakini mpaka hivi sasa anamiliki Magari manne ya kifahari na nyumba nne.

Baada ya Lynn kuonekana akipiga picha na magari hayo na hata kwenye nyumba hizo tetesi zilianza alidaiwa kwa kuazima magari na hata nyumba sio mali zake.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Lynn aliweka hati zake zote za magari ili Kudhihirisha kuwa yeye ndio mmiliki halali wa magari yake yote:

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Lynn amewatolea povu mashabiki ambao wamekuwa wakimtuhumu kwa kujionyesha na mali ambazo si zake

Ndiyo mali ni za kwangu. Mbona huwa ninaposti mitandaoni na hati zake kama hati za nyumba na magari yangu? Ninaponunua magari kwani huwa hamuoni? Tena hivyo ni baadhi tu maana nina nyumba nne na magari manne. Pia jumlisha na gari lingine nililonunuliwa Jumanne (wiki hii) na nimeposti kadi ya gari ikiwa na jina langu, sasa ni ukweli gani ambao watu wanataka kujua kutoka kwangu?.

Unajua kinachowauma watu ni kwa sababu ninamiliki vitu vingi vya thamani halafu ndiyo kwanza nina umri wa miaka kumi na nane, nimewapita hadi niliowakuta wakiwika mjini, kiukweli inauma na hata ningekuwa mimi ningeumia kama wanavyoumia, ila sidangi jamani nina ishu zangu kibao ninafanya hapa mjini halafu naona watu wananichukulia poa kama wanaona kudanga rahisi si wadange na wao (alicheka na kukata simu).”.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.