Lynn Aweka Mitandao Ya Kijamii Kando Ili Kufanya Mambo Ya Msingi

Video vixen maarufu aliyegeukia muziki wa  Bongo fleva hivi karibuni Irene Charles maarufu kama Lynn amefunguka na kusema kuwa hivi sasa ameamua kuachana na Mitandao ya kijamii.

Lynn ambaye alikuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz na kusababisha kukamata headlines kila siku Mitandaoni Lakini tangu mahusiano hayo yaishe Lynn amekuwa kimya sana.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa, Lynn alisema watu wengi sasa wamegundua kuwa maisha ya mitandaoni yanadanganya na kama mtu asipokuwa makini, hawezi kufanya chochote cha maana zaidi ya kudili na mitandao ya kijamii.

Nilikaa na kuwaza kuhusiana na maisha ya mtandaoni maana yanaweza kukufanya ukawa bize bila sababu ya msingi hivyo hata ukiniona kwenye mitandao ni kwa sababu maalum tu“.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.