Loading...

M-Rap Atangaza Kuwa Anatafuta Mchumba

July 11, 2018 at 08:25
M-Rap Atangaza Kuwa Anatafuta Mchumba

Msanii wa muziki wa Bongo fleva anayefanya miondoko ya kurap na anayetamba na ngoma yake mpya ya ‘Nairobi love’, M-Rap amefunguka na kusema anatafuta mchumba.

M-Rap amefunguka na kudai baada ya kuwa Single Boy kwa muda mrefu hatimaye yupo tayari kuwa na mwenza wake ambapo amesema shanti awe na miaka 18 kwenda juu.

Loading...

Kwenye Interview yake na Enews ya East Africa Tv, M-Rap alifunguka haya kuhusu mwanamke ambaye anamtafuta ili awe mpenzi wake:

Mimi natafuta msichana ambaye ninaweza nikakaa na nikatulia naye naweza kusema natafuta Wife material kwani nimekuwa nikimtafuta huyo msichana kwa sababu wasichana wengi ninaokuwa nao wanakuwa na drama nyingi mwisho wa siku naachana nao.

Lakini M-Rap aliendelea kufunguka:

Kwaiyo kwa msichana yoyote anayehisi anaweza kuwa na mimi atanitafuta kupitia page zangu za mitandao ya kijamii Kwenye Facebook, Twitter na Instagram.

Sina vigezo vingi ila awe msichana mwenye tabia nzuri, mwenye kuanzia miaka kumi na nane na kuendelea ila asiwe bibi na pia awe anafanya kazi”.

 

Share

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment

Loading…