Loading...

Mabeste Awatolea Povu Wanaodhalilisha Wanawake

November 08, 2018 at 12:51
Mabeste  Awatolea Povu Wanaodhalilisha Wanawake

Msanii wa muziki wa kizazi kipya wa siku nyingi MABESTE amefunguka na kutoa dukuduku lake la moyoni kuhusu baadhi ya wanaume wanaokaa kutwa kuwadhalilisha wanawake wanaokuwa nao katika mahusiani hata kama wanakuwa tayari wameshaachana nao.

Mabeste anasema kuwa wanaume wamekuwa na tabia ta kuwadhalilisha sana wanawake wao huku akisema kuwa ameumizwa  sana na swala la wema na PCK.

Loading...

Mabeste anasema kuwa kwa muda sasa mambo kama haya yamekuwa yakitokea na wamekuwa wakitasikia lakini ifike sehemu inabidi wanaume wajifunze kuwaheshimu na kuwapenda wanawake zao kama vile ilivyokuwa kwa mamamzao na hata dada zao wanapokuwa nyumbani.

Mabeste anasema kuwa wanawake ni zaidi ya ndugu kwa sababu mpaka mnaamua kuwa mwili mmoja kuna vitu vingi mnakuwa tayari mmeshajitoa kuvifanya hivyo ni vizuri kuwaheshimu, hata hivyo mabeste anasema kuwa ikitokea mnaamua kuachana basi ni bora kuachana kwa amani na kila mmoja afanye mambo yake.

Mabeste ni moja ya wasanii waliokaa katika ndoa kwa muda mrefu na kupoitia magumu mengi na mama watoto wake lakinikila siku amekuwa akimuweka mke wake katika  kipaumbele cha maisha yake.

 

 

Share

Comments

  1. Louder

  2. Mwenye sikiona na asikie

  3. Washenzi ndivyo walivyo

  4. Mawaidha mazuri sana

  5. Nice…

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment

Loading…