Mabeste Awatolea Povu Wanaume Wanaodhalilisha Wanawake

Msanii wa muziki wa Bongo fleva aliyewahi kutawala kwenye gemu Venance William maarufu Kama Mabeste amewaji juu wanaume ambao wanadhalilisha wanawake.

Mabeste amezungumza hayo Baada ya kuwepo matukio mengi ya wanaume kudhalilisha wanawake waliozaa nao au waliokuwa nao likiwemo lile la muigizaji Wema Sepetu na mpenzi wake PCK.

download latest music    

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Mabeste alisema kuwa, vijana inabidi wajitambue na kuwaheshimu wake zao kama ambavyo wanawapenda na kuwaheshimu mama zao kwa sababu wanastahili heshima na thamani.

Unapomdhalilisha mke wako au mwanamke wako ni sawa na umejidhalilisha mwenyewe kwa sababu mwisho wa siku nyie ni mwili mmoja, kama mnafikia uamuzi wa kuachana achaneni kwa amani sio mpaka kila mtu ajue majirani au mitandaoni”.

Msanii mkubwa Kama Diamond Platnumz ameshawahi kunyoshewa kidole kwa kudhalilisha wanawake aliozaa nao Baada ya kuweka video na picha za faragha Waliowahi kuwa wapenzi wake Hamisa Mobetto na Zari.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.