Madame Ritha Afunguka kuhusu Harmonize

Ritha Paulsen au maarufu kama “Madam Ritha” amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu Mwanamuziki Harmonize ambaye aliwahi kuwa mshiriki katika shindano la kusaka vipaji la Bongo Star Search.

Madame Ritha ambaye alikuwa mwanzilishi wa shindano hilo la Bongo star search na chief judge ambalo lilikuwa limejikita katika kutafuta vipaji vipya vya waimbaji wapya. Harmonize ambaye kwa sasa ni mmoja kati ya wasanii wanaofanya vizuri kwenye bongo fleva chini ya lebo yake ya Wasafi CB. Kabla ya kupata nafasi ya kuwa msanii chini ya lebo hiyo, Harmonize alienda kujaribu nafasi yake katika mashindano hayo ambayo hakufanikiwa kufika mbali kwa kile alichokidai Madam Ritha kuwa hakuimba vizuri.

download latest music    

Madame Ritha amemsifia Harmonize kwa mafanikio yake na kukiri kuwa yeye ni mmoja kati ya watu waliompa changamoto ya kufanya vizuri kwani kwa kipindi kile alikuwa hafanyi vizuri kama sasa Madam Ritha amesema  yafuatayo:

“Alikuja Harmonize kwenye Bongo Star Search na kama tusingemnyoosha wakati ule, May be asingekuwa bora leo na kwenye label kubwa ya muziki hapa nchini. Harmonize alikuwa anaimba “MARAIKA”, hata ingekuwa wewe usingempokea awe msanii wako na ujivunie”.

Harmonize aliwahi kuwafariji watu kuwa wasikate tamaa wakikosea mara moja kwenye maisha kwani yeye angekata tamaa alipokosolewa kwenye BSS basi asingefika pale alipo leo, kwa sasa Hamonize anatamba na nyimbo zake zinazofanya vyema redioni kama “Nimechoka”, “Bado” na vinginevyo vingi.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.