Makala Aelezea Uhusiano Wake na Odama.

Mtayarishaji wa filamu nchini Tanzania Makala amefunguka na kuelezea mahusiano yake na mwanamaigizo na mtayarishaji mwenzake  Jenipher  Kyaka almaarufu kama Odama  kuwa wanamahusiano ya kikazi zaidi kwa sababu wote wanafanya kazi za sana na kwamba wote walikuwa zao kubwa kutoka kwa musa banzi amabe aliwatoa wasanii wengi chipukizi miaka ya nyuma.

Makala anasema kuwa watu wengi wa bongo wamekuwa na tabia ya kuzusha mambo bila kuwa na uhakiaka na kile wanachokiongea na yeye hana kitu chochote kinachoendelea kati yao.

download latest music    

Unajua kuwa wabongo wamekuwa wakizungumza mambo mengi sana, na hawajui mimi na odama tumetoa  wapi, na wameanza kusambaza ujumbe kuwa nina mahusinao nae ya kimapenzi, taarifa hizo sio za kweli na hawana hata uhakika nazo na laiti wangejua mimi na Odama tuko aje wasingeongea kabisa, maana Odama ni kama nimezaliwa nae tumbo moja na ninajiskia vibaya sana.

Makala anasema kuwa pamoja na yote lakini Odama kwake ni moja ya watu waliochangia sana mafanikio yake makubwa aliyonayo sasa kwahio anaomba watu wanapokuwa wanataka kuongea waongee kitu kinachoeleweka na chenye uhakika.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.