Mama Diamond na Zari Wadaiwa Kuwa Ndani Ya Bifu Zito

Mama mzazi wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Bi. Sandrah au maarufu kama Mama Diamond amedaiwa kuwa kwenye bifu zito na mazi mwenzake na mwanaye mwanamama Zari The Bosslady.

Global Publishers wanaripoti kuwa kuna bifu zito linaendelea kati ya Zari na Mama Diamond huku mtu wa karibu na familia hiyo kuanika kuwa wawili hao waliingia kwenye mgogoro baada ya mama Mondi kubeba ujauzito.

download latest music    

Inaripotiwa kuwa Mama Mondi alipata ujauzito na kumueleza mkwewe huyo kuwa anahitaji daktari mzuri kutoka Afrika Kusini ili ahakikishe kuwa ujauzito huo hautoki kwani anahitaji kupata mtoto na mumewe Maisala Shante ‘Anko’ ili aifurahie ndoa yake.

Unajua kwa nini mama Mondi na Zari waliingia kwenye bifu akamchukia? Ni kwa sababu alimpa siri ambayo alikuwa hajamwambia mtu yeyote ya ujauzito wake yeye akamwambia meneja mmoja wa Diamond ambaye naye alimtania mama bila kujua kuwa ilikuwa ni siri”.

Aidha, mtoa habari huyo alisema kuwa baada ya Zari kumueleza meneja huyo bila kujua kuwa hakutaka mtu ajue na meneja huyo akamtania mama Mondi kuwa ni mama kijacho kitendo ambacho kilimkera ndipo bi’mkubwa huyo alipomchamba Zari.

Unaambiwa mama Mondi alimchamba Zari vibaya na bahati mbaya ujauzito wenyewe ukatoka kwani ulitoka hata kabla hajapata msaada aliokuwa anautaka”.

Baada ya tetesi hioz za bifu na Zari gazeti la Amani lilimsaka Mama Diamond ambaye alikana kabisa bifu hilo na mkwe wake na kufunguka;

Sina bifu na Zari mbona huwa nawasiliana naye kwa njia ya WhatsApp na mara ya mwisho amenitumia picha za watoto na kuhusu kumposti kwenye Instagram mbona tulishaacha kupostiana siku nyingi ndio maana sijamposti lakini hatuna bifu lolote“.

Mama Diamond alipoulizwa kuhusu taarifa za ujauzito alidai kwamba ameshezaa tayari na kwa sasa mtoto wake ameshakuwa mkubwa tuu.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.