Mama Kanumba Analia Njaa kwa Sababu ya Movies za Mwanae.;-Ray kigosi

Msanii Ray kigozi amefunguka leo akiwa katika conference ya kutambulisha movie yake mpya, Ray anasema kuwa pamoja na kwamba kuna utambulisho wa movie hiyolakini pia wameamja kuingia mkataba na kampuni nyingine kubwa itakayo husika na kusambaza movies nchini lakini movies hizo zitabaki  kuwa mali ya msanii na sio kampuni.

Akitoa sababu ya kuamua kungia katika kampuni hiyo, Ray anasema kuwa ni kwa sababu wasanii wengi wamekuwa wakiingia mikataba na kampuni ambazo zinakuwa  zinachukua mamlaka ya movies zote bila kumpa msanii haki zake.

download latest music    

Akimtolea mfano, mama yake mzazi na marehemu Kanumba, Ray anasema  kuwa mama kanumba kwa sasa amekuwa akilia na kuangaika na maisha magumu kwa sababu haki za filamu zinabaki kwa wahindi.

Mama Kanumba amekuwa akilia njaa kila siku kwa sababu filamu za mtoto wake zote ziko chini ya mamlaka ya wahindi,lakini hii kampuni ni mpya na itakuwa ikifanya kazi kwa miezi sita baada ya hapo mali inabaki kuwa ya msanii.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.