Mama Kanumba Ateta Na Wanaomwita Hamisa Mnafiki

Ni siku kadhaa zimepita tangu Hamisa Mobeto  kuandika na kusema hisia zake katika vyombo vya habari kuhusu huzuni aliyokuwa nayo kuhusu hukumu aliyoipata msanii wa bongo movies Lulu Michael baada ya kukutwa na hatia ya kuua bila kukusudia.

Katika baadhi ya mahojiano yake Hamisa alisema kuwa pamoja na kwamba amekuwa katika mahusiano mabaya na Lulu kwa muda mrefu kabla ya kupatwa na hayo matatizo lakini hii haimfanyi yeye kumchukia Lulu kwa sababu alikuwa mama bora kwa mtoto wake aliezaa na Majizzo ambae kwa wakati huo mwanaume huyo alikuwa katika uhusiano wa kimapenzi na Lulu Michael.Hamisa pia alisema kuwa haitakuwa busara kumchukia lulu wakati Lulu alikuwa akikaa na mtoto wake vizuri na hata sasa hivi mtoto huyo amekuwa akimuulizia sana.

download latest music    

Hata hivyo wiki hii mwishoni kulikuwa na uzinduzi wa filamu ya Zero Player ambayo Hamisa Mobeto pia alikuwa ni mmoja wa waigizaji, katika uzinduzi huo mama mzazi wa marehemu Kanumba alikuwepo pia katika uzinduzi huo kwa sababu mdogo wake na marehmu Kanumba pia alikuwa na mmoja wa washiriki katika filamu hiyo hivyo wawili hao walipata kukutana.

Baada ya Mama Kanumba na Hamisa kuonekana katika piacha za pamoja baadhi ya watu wametokwa na mapovu na kusema kuwa Hamisa amekuwa mnafiki kwa sababu  kwa maneno aliyoyaongea Mama Lulu kuhusu Lulu yalionesha kuwa anachuki na Lulu sasa inakuwaje tena Hamisa anakuwa karibu na Mama Kanumba kama alisema kuwa hana chuki na Lulu ilhali  Mama Kanumba hapatani na Lulu?

Mama Kanumba baada ya kusikia maneno hayo aliamua kuwajibu mashabiki na kuwaambia kuwa Hamisa Mobeto hana unafiki wowote na anavyojua yeye watu hao wawili wote ni watoto wake.

Sioni haja ya watu kumsema vibaya Hamisa na kumuita mnafiki,wote hao ni watoto wangu nahakunahaja ya kumuona Hamisa mnafiki bwana. Alisema Mama Kanumba

Mwishoni mwa wiki hii ulifanyika uzinduzi wa filamu ambayo inasemekana kupokelewa vizuri na mashabiki wa Hamisa Mobeto na hii itafunguka sura mpya ya msanii Hamisa katika uwanja wa filamu na bongo movies kwa ujumla.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.