Mama Lulu Afungukia Hali Yake Baada Ya Hukumu Ya Mwanae.

Ni wiki sasa imepita tangu Lulu Micheal ahukumiwe kwa kesi yake ya kuua bila kukusudia.Mama mzazi wa msanii huyo amefunguka na kuonglea hali yake aliyonayo tangu alipokea kifungo hicho.Mama wa msanii huyo hakuwahi kuongea kitu chochote tangu mtoto wake apelekwe jela pamoja na kwamba kulikuwa na maneno ya kumtuhumu mama na baba wa Lulu kuwa hawakuwahi kumpa Lulu malezi bora yaliyompelekea kufanya vitu vya ajabu.

Ijumaa wikienda, liliamua kumtafuta mama yake mzazi na Lulu  Michael, na kumuuliza hali yake na jinsi gani aliweza kupokea hukumu ya mwanae.Hata hivyo mama huyo alisema kuwa kwa sasa hawezi kuongea kitu chochote kwa sababu hata yeye hajisikii vizuri na hali yake hata kiafya haijatengema kwa sababu kama mzazi hawezi kuwa sawa hata siku moja.

download latest music    

Nafikiri kwa kipindi hiki nahitaji zaidi kupumzika zaid kuliko kuwa naongeaongea, sipendi kuzungumza hovyohovyo na  kwakweli siko vizuri kabisa tangu mwanangu afungwe.

Najua watu wamekuwa wakinishangaa kwanini nimekuwa kimya kwa muda mrefu lakini ukweli ni kwamba hata hali yangu haiko vizuri kabisa,na sidhani kama kuna mtu au mzazi yoyote ambae hataweza kuwa sawa kutokana na hali ya matezo anayokutana nayo  mtoto wake anapokuwa kule tena ni matso ambayo alishawahi kuyapitia, kwakweli ninaumia sana sana.

Lakini pia waandishi wa habari hawakuishia hapo waliamua kuwatafuta baadhi ya madaktri ili kuweza kuzungumzia ni kitu gani kinaweza kumpata mtu anaekutana na mateso  na hali ngumu ya maisha  ukizingatia Lulu ni msichana mdogo ambae alishayapia hayo na anakutana nayo tena kwa sasa.

Moja ya wataalamu wa afya anasema kuwa uwezekana wa Lulu kuugua ni mkubwa kwa sababu ya kuwa na msongo wa mawazo  ambao pia usababisha kwa kiasi kikubwa  mpangilio mbovu wa homoni  a hata kusababisha mtu kuchanganyikiwa kwa sababu ya kuwa na upweke muda mrefu na kuwa na mgandamizo wa hisia (depression).

Lulu alipokea na kuanza hukumu yake mara tu alipoipokea kutoka mahakamani hapo tarehe 13 Novemba mwaka huu , baada ya kukutwa na hatia ya kuua bila kukusudia kwa msanii mwenzie Steven Kanumba ambae alikuwa ni mpenzi wake.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.