Loading...

Mama Yangu Hataki Kabisa Niimbe- Nay Wa Mitego

October 12, 2018 at 13:37
Mama Yangu Hataki Kabisa Niimbe- Nay Wa Mitego

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Emanuel Elibariki maarufu kama Nay wa Mitego ameibuka na kuweka wazi kuwa Mama yake mzazi hataki kabisa aimbe kutokana na changamoto alizowahi kumbana nazo.

Nay wa Mitego ambaye anafanya vizuri na ngoma yake ya ‘Alisema’ amewafungukia Global Publishers kuwa mama yake mzazi amemtaka kuachana na muziki na kuangalia biashara nyingine.

Loading...

Mama yangu hataki nifanye muziki na niendelee kuimba kwa sababu ya matatizo ninayokutana nayo katika kazi zangu kwa sababu mara ya mwisho nilipokamatwa baada ya kutoa Wimbo wa Wapo ndiyo alinikataza, aliniambia niachane na muziki nifanye shughuli nyingine maana nitakuja kufa siku si zangu.

Huu wimbo nimefanya kwa ajili ya wananchi wa Tanzania na mashabiki wa muziki wangu, nimefanya kwa ajili ya hali iliyopo kwa sasa, ninampenda sana mama yangu na huwa ninamsikiliza sana, lakini kwa Wimbo wa Alisema nilijua tu unaweza kuzua balaa (utata), lakini nilipokuwa nikiendelea na kukumbuka kauli ya mama wakati nimeingia studio na kurekodi ndiyo nikaambiwa hebu weka sawa mashairi yako na ndipo nikayapangilia na wimbo ukatoka kama mnavyousikia.

Kwa kuwa nilimuahidi mama kuwa sitafanya muziki anaonikataza, kwa hiyo kwenye huu wimbo najua yeye asingeukubali utoke ndiyo maana nikamwambia mama huu ni wa mwisho naapa”.

Nay Wa Mitego amesema ataacha kuimba nyimbo ambazo zinaikosoa serikali na zenye utata lakini ataendelea kuimba nyimbo za kawaida kwani muziki ndio unamuongizia kipato hivyo hawezi kuacha kabisa.

Share

Comments

  1. Mama knows best

  2. She had your best interests at heart

  3. 😭😭😭😭😭😭

  4. Jameni mwenyezi Mungu atulindie Mama zetu na awape maisha marefu

  5. Anakutakia mema tu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *


in Entertainment

Loading…