Mamia Wampongeza Diamond na Zari

Jana  Septemba 19 katika kurasa nyingi za mtandao ya Instagram kulikuwa kulikuwa kukipostiwa picha za Diamond huku wakimpongeza kwa hatua nzuri aliyoichukua ya kukubali kuwa yeye ndie  baba kwa mtoto wa Hamisa.

Diamond ambae siku ya jana alikuwa akiongea na waandishi wa Leo tena katika Television ya Clouds, aliamua kufunguka na kusema ukweli kuwa alikuwa na mahusiano na mwanadada mrembo Hamisa Mobeto na amepata nae mtoto ,tetesi ambazo zilikuwepo kwa muda mrefu na Diamond  Alikuwa akipinga tetesi hizo kwa mara ya kwanza.

download latest music    

Baada ya Diamond kukubadi kuwa Abdul Naseeb ni mtoto wake baadhi ya viongozi walimpongeza Diamond kwa hatua hiyo.Baadhi ya viongozi hao ni pamoja na mheshimiwa mkuu wa mkoa wa Dar Es Saalm Paul Makonda “Thamani yako kwangu bado ni kubwa sana , kwani uwezo wako wa kupita kwenye dhoruba na ukabaki imara na familia yako unaendelea kukupa heshima”.aliandika hivi kwa Zari

Pia mbunge wa Mikumi mh. Joseph Haule aliandika hivi “Ukweli humuweka Mtu huru kweli kweli, Big up mdogo wangu @diamondplatnumz Umekuwa Mfano bora sana,”

Ukiachana na viongozi kuna wasanii kama Bactuli Actreess , Faiza ally, Tanzanian Sweetheart Wema Sepetu , ukiachana na kuwa alikwishaachna na Diamond lakini pia alimpongeaza na kuandika”he is such a brave soul”  pia hakuacha kumpa heshima yake Zari The Bosylady ambae ndio mama halali wa watoto wawili  na anaejulikana kwa diamond ,ukiachana na kwamba kiindi cha nyuma wawili hao wawikuwa katika migogoro pia.

Diamond alichukua uamuzi wa kukubali mtoto wa hamisa baada ya kuzongwa kwa muda mrefu na maneno ya mitandaoni,lakini pia picha zilizovuja zikiwaonyesha yeye na hamisa wakiwa chumbani.Hata hivyo Diamond amekubali kosa ilo na kuiomba msamaha familia yake kwa kudhalilika katika mitandao kwa sababu ya ujinga wake.Lakini pia Diamond amemtaka hamIsa kufikiria biashara ya kufanya ili kumsaidia yeye na mtoto huyo, pia Diamond amehakisha kuwa yeyey na Zari hawataachana yuko radhi kupiga magoti Tanzania mpaka Afrika ya Kusini kuomba msamha kwa Zari.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.