Maneno ya Mitandao Yamrudisha Nyuma Steve Msiba wa Godzilla

Maneno ambayo yamekuwa mengi katika mitandao ya kijamii kuhusu msanii Steve Nyerere kuwa akitumia sana misiba na kupata michango ambayo mwisho wa siku inakuwa ikimnufaisha mwenyewe  imekwamisha maswala mengi sana katika kufanikiwa katika mazishi ya wasanii wengi na hata huu wa msanii Godzilla.

Steve Nyerere kwa sasa amekuwa kimya na amekuwa kama muuzuliaji tu katika misiaba na kujiweka pembeni ilhali kulikuwa na haja ya kujihusisha na misiba ya wasanii wenzake kwa sababu amekuwa na ushawishi mkubwa katika kufanikisha mambo mbalimbali.

download latest music    

Msanii huyo alipopata taarifa za msiba wa Godzilla , hakutaka kujihusisha sana zaidi ya kuonyesha kuwa hata yeye ameguswa na msiba na kuamua kuweka post kaushiria pole yake kwa familia kumpoteza msanii huyo lakini bado  wapo walioamua kumshambulia msanii huyo na kumwambia kuwa amekuwa akijinufaisha na misiba.

Hata hivyo umuhimu wake unaonekana kwa sababu bado wapo wanaohitaji msaada wake katika misia ba hata huu wa Godzilla lakini amekuwa kimya na hataki kujihusisha na kitu chochote.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.